Mkuu wa chama cha upinzani cha Afrika kusini Julius
Malema na wabunge wake 11 wamesimamishwa katika bunge bila malipo baada ya
kumdhalilisha rais wa nchi hiyo.
Wakati Rais Jacob Zuma alipolihutubia bunge mwezi Agosti, wanachama wa Economic Freedom Fighters (EFF) walipiga kelele wakisema "lipa pesa zetu".
Walikuwa wakimaanisha matumizi ya dola milioni 23 ya pesa za serikali kukarabati nyumba yake binafsi huko Nkandla.
Mapema mwezi huu, bunge lilimfutia makosa.
Chama hicho cha EFF kilisema kitapambana mahakamani kusimamishwa huko, ambapo ni kati ya siku 14 hadi 30.
No comments:
Post a Comment