Tuesday, 25 November 2014

MAHAKAMANI KWA KUMFANYA BINTI KUWA 'MWEUPE'





 






















Halle Berry amempeleka aliyekuwa mpenzi wake Gabriel Aubry mahakamani kwa madai ya kutaka kubadilisha muonekano wa binti yao ili awe mweupe.

Anadai Aubry amezinyoosha nywele za Nahla zilizojinyonganyonga na kuzipaka rangi kwa nia ya kumfanya asionekane Mmarekani mweusi.

Nyaraka za mahakamani zinamshutumu Aubry kwa kumsababishia “uharibifu wa kisaikolojia na wa mwili” kwa binti yao mwenye umri wa miaka sita na kumsababishia aanze kuwaza “kwanini muonekano wake wa asili hautoshi ”.

 “Nataka mimi na Gabriel tuchukue uamuzi pamoja juu ya binti yetu, ukuaji wake, maendeleo yake na maisha yake kwa ujumla,” alisema Berry kwenye nyaraka hizo.

Wakili wa Berry, Steve Kolodny, ndie aliyekuwepo mahakamani siku ya Jumatatu pamoja na Aubry.
Jaji alitoa uamuzi kuwa hakuna mzazi hata mmoja anayeweza kubadili muonekano wa Nahla kutoka asili yake.

Wapenzi hao waliachana mwaka 2010 baada ya kuwa pamoja kwa miaka minne.


Chanzo: www.independent.co.uk
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
 

No comments:

Post a Comment