Bi Janina aliwekwa chumba cha kuhifadhia maiti kabla ya wakati wake |
Mwanamke mmoja raia wa Poland mwenye umri wa miaka 91 aliyekaa chumba cha kuhifadhia maiti kwa saa 11 baada ya kutangazwa kufariki dunia amerejea kwenye familia yake, akilalamika kusikia baridi.
Maafisa walisema Janina Kolkiewicz alitangazwa kufa baada ya dakatari wa familia kumfanyia vipimo.
Hata hivyo, wafanyakazi wa chumba hicho cha kuhifadhia maiti walishtuka kuona mfuko maalum alimohifadhiwa ukitikisika. Polisi wameanza uchunguzi.
Aliporejea nyumbani, Bi Kolkiewicz alipata joto kwa kunywa bakuli la supu na mikate ya maji miwili.
Familia yake na daktari walisema wameshtushwa na jambo hilo.
Mtoto wa kike wa ndugu wa bibi huyo, katika mji wa Ostrow Lubelski, mashariki mwa Poland alimwita daktari huyo baada ya kurudi nyumbani asubuhi moja na kumkuta shangazi yake hapumui na mapigo ya moyo yamesimama.
Baada ya kumpima bibi huyo, daktari alimwambia ameshafariki dunia na kumwandikia cheti cha kifo.
Mwili ukapelekewa chumba cha kuhifadhia maiti na maandalizi ya mazishi yalikuwa yafanyike baada ya siku mbili.
Cheti hicho sasa kimetangazwa kuwa batili, gazeti la Dziennik Wschodni limeandika.
Bi Kolkiewicz hana habari ni kwa kiasi gani alikaribia kuzikwa hai, kwani binti yake alisema ana ugonjwa wa kusahau.
No comments:
Post a Comment