Wanawake
wawili wa kujitoa mhanga wamejilipua kwa mabomu katika soko lenye mkusanyiko wa
watu wengi katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifo
vingi, walioshuhudia walisema.
Takriban
watu 30 waliuawa baada ya vijana hao
wawili walipojilipua, walioshuhudia waliwaambia shirika la habari la AP.
Mmoja
aliyeshuhudia Sani Adamau aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mlipuko
wa pili ulitokea watu walipokuwa wanajaribu
kuwasaidia wale waliojeruhiwa kwenye mlipuko wa kwanza.
Kundi la wapiganaji la Boko Haram limeshafanya
mashambulio mengi Nigeria.
Kundi
hilo lilianzia Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno, baada ya kuundwa mwaka
2002, lakini tangu wakati huo limefurumushwa mjini humo na jeshi pamoja na
makundi ya sungusungu.
Sasahivi
linadhibiti maeneo makubwa ya miji na vijiji huko Borno, huku kukiwa na hofu ya
kuiteka Maiduguri.
Boko
Haram halijasema lolote kuhusu shambulio hili.
No comments:
Post a Comment