Sunday, 30 November 2014

MAVAZI YA MABINTI WA OBAMA YALETA KIZAAZAA



 US President Barack Obama smiles at his daughters Sasha and Malia after he pardoned a turkey during a ceremony at the White House on 26 November 2014 in Washington



Mabinti wa Rais Barack Obama Sasha na Malia wameelezewa na afisa mmoja wa chama cha Republican kukosa heshima na hadhi kutokana na mavazi yao siku ya sherehe za Thanksgiving.

Elizabeth Lauten, mkurugenzi wa mawasiliano wa mbunge wa Republican Stephen Fincher, aliandika kauli hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kauli yake hiyo ilikoselewa na wengi na hatimaye kufutwa.

Bi Lauten ameomba radhi kwa “maneno yake yaliokera.”

Aliwashambulia mabinti hao kutokana na mavazi waliovaa katika shughuli ya kila mwaka iliyofanyika Ikulu ya White House.

Malia, mwenye umri wa miaka 16, na Sasha, 13, walisimama karibu na baba yao siku ya shughuli hiyo.

Bi Lauten alisema mabinti hao wangejitahidi "kuonyesha hadhi kidogo".

"Vaa kama unastahili heshima, sio kama uko baa," aliongeza.

Kauli zake hizo zilisababisha hamaki kwenye mitandao ya kijamii, huku kukiwa na madai kuwa alikuwa “akiwadhalilisha” mabinti hao vijana.

Chanzo: washingtontimes.com

No comments:

Post a Comment