Saturday 22 November 2014

KIFO CHA MTOTO KILICHOZUA HASIRA, UGANDA



Man holding the body of Ryan Ssemaganda
Mwili wa Ryan Ssemaganda (uliobebwa) ulizikwa nyumbani kwao nje kidogo ya Kampala

 Mazishi ya mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili yamefanyika Uganda,

Kifo chake kiliamsha hamaki kufuatia hatua ya kugongwa na gari la manispaa ya jiji la Kampala baada ya mama yake kukamatwa kwa kuuza matunda kinyme na sheria.

Familia ya Ssemaganda na wanasiasa wa upinzani walitishia kutomzika hadi maafisa wakiri kuhusika na kifo chake.

Mwili wa marehemu ulipelekwa bungeni siku ya Alhamis kuonyesha kupinga kwa tukio hilo.

Waganda wengi wanahisi manispaa ya jiji la Kampala linawaonea sana wachuuzi.

Mkasa mzima

Mama yake alikamatwa siku ya Jumatatu kwa kuuza matunda mitaani bila kibali.

Siku iliyofuata, bibi yake alimchukua mtoto huyo kwenye ofisi za Mamlaka za Mji Mkuu Kampala (KCCA), alipokuwa amewekwa kizuizini mama huyo, ili aweze kumnyonyesha.

Ryan Ssemaganda's mother (right)
Mama yake Ryan Ssemaganda( kulia) sasa ameachiliwa huru 

Maafisa wa KCCA inaripotiwa walimkatalia, lakini wakati majadiliano yanaendelea, alimponyoka bibi yake na kugongwa na gari la KCCA.

Siku ya Alhamis polisi walizuia mwili wa mtoto huyo kupelekwa bungeni.

"Hatutaki maiti bungeni. Nendeni mkamzike, msivuruge amani ya maiti," alisema kamanda wa polisi wa kanda hiyo James Ruhweza, kulingana na gazeti la Monitor.

Alisema dereva wa gari hilo atafunguliwa mashtaka na kuisihi familia isiruhusu wanasiasa kuwatumia kutokana na tukio hilo.

Mwanasiasa wa upinzani Erias Lukwago alitembelea familia hiyo kabla ya kuchukua mwili wa mtoto huyo bungeni, gazeti la Monitor limesema.


No comments:

Post a Comment