Polisi wa kuzuia ghasia Afrika kusini
wamepambana na wabunge wa upinzani saa chache baada ya bunge kumfutia rais
Jacob Zuma tuhuma za matumizi ya dola milioni 23 za fedha za taifa kukarabati
nyumba yake binafsi huko Nkandla.
Waliingilia kati baada ya mbunge wa upinzani Ngwanamakwetle
Mashabela kurudia mara kwa mara kumwita Bw Zuma mwizi.
Wabunge wanne walijeruhiwa katika tafrani hiyo
iliyotokea katika kikao cha usiku.
Mwezi Machi, mchunguzi wa ufisadi nchini humo alisema Bw Zuma ‘alifaidika kupita kiasi’ kutokana na ukarabati huo.
Mwezi Machi, mchunguzi wa ufisadi nchini humo alisema Bw Zuma ‘alifaidika kupita kiasi’ kutokana na ukarabati huo.
Mwendesha mashtaka Thuli Madonsela pia
alimshutumu kwa kukiuka maadili na kupendekeza alipe fedha zilizotumika kukarabati
vitu visivyohusiana na masuala ya usalama huko Nkandla, kwenye jimbo la KwaZulu
Natal, lililo na bwawa la kuogelea na mabanda ya mifugo.
Nyumba yake binafsi ina bwawa la kuogelea na mabanda kadhaa ya mifugo |
Lakini ripoti ya kamati ya bunge –
iliyopitishwa na wabunge walio wengi kutoka chama cha African National Congress
(ANC) siku ya alhamis- imemsafisha Bw Zuma kuwa na kosa lolote.
Serikali nayo pia ilisema ilibidi fedha hizo
kutumika kwa minajil ya usalama.
No comments:
Post a Comment