Sunday 16 November 2014

AAMBUKIZWA HIV KWA 'MANICURE' ?



 
Kwa wanawake wengi, jambo baya linaloweza kumtokea katika saluni ya kutengenezea kucha ‘manicure’ ni labda wamechagua rangi mbaya ya rangi wakaishia kujuta, au kucha kukatwa sana.

Lakini kwa binti mmoja mwenye umri wa miaka 22 nchini Brazil, ukataji na urembaji huo wa kucha uligueka mtihani: Uamuzi wake huo huenda umemwambukiza virusi vya HIV.

Binti huyo ambaye tukio lake limeelezwa katika jarida la AIDS Research and Human Retroviruses, amekutwa hivi karibuni na ugonjwa wa ukimwi wa kiwango cha juu lakini bado haijulikana kaambukizwa vipi hasa katika mazingira yanayojulikana kawaida – hajawahi kufanya mapenzi, kuingiziwa damu au kufanyiwa upasuaji, au hata kutobolewa masikio.

Madaktari wamechanganyikiwa wasijue aliambukizwa vipi virusi vya ugonjwa huo.

Baada ya kuthibitisha madai yake hayo, madaktari wake wakazidi kuchimba ukweli, ili kutambua tukio lolote ambalo lingeweza kumwambukiza.

Njia pekee: mgonjwa huyo alikumbuka aliwahi kutumia vyombo vya kutengeneza na kupamba kucha na ndugu yake  miaka 10 iliyopita.

Ndugu yake huyo alikuwa akifanya biashara ya kutoa huduma za kutengeneza na kupamba kucha ambaye baadae aligundulika kuwa na virusi vya HIV.

Baada ya uchambuzi wa kina wanawake wote wawili, walikuwa na virusi vya aina moja, na kusababisha watafiti hao kufikia muafaka wa kwamba vyombo vya kufanyia kazi hiyo ni njia ya kueneza virusi vya HIV.

 Licha ya kuwa wengi hawatumii mkasi mmoja na mtu aliye na virusi vya HIV, wanawake wengi na baadhi ya wanaume- huenda wameshatengenezwa kucha kwenye saluni, ambapo vyombo hivyo hutumika mara kwa mara.

Nchini Marekani njia ya kusafisha vyombo hivyo hutofautiana jimbo hadi jimbo, japo maeneo mengi huosha vyombo hivyo kwa maji na sabuni, huziloweka kwenye dawa ya kuua vijidudu kwa dakika 10 hadi 30, kusuuza vyombo hivyo kwenye maji masafi na kukausha kwa kitambaa, kisha kuhifadhi kwenye sehemu safi na kuzifunika.

Chanzo: yahoo.com                         
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

1 comment:

  1. hii inaonyesha kuna njia nyingi za kupata maambukizi, wengi wetu huwa tunakimbilia kuwa mwenye HIV ni asherati,mzinzi wa kutotumia kinga za maradhi lakini kwa hili inaonyesha unaweza kuwa muangalifu lakini ni bahati mbaya tu ndio mstari unaotenganisha katika kupata au kutokupata maambukizi.

    ReplyDelete