Saturday, 1 November 2014
POLISI WA KENYA 'WAUAWA TURKANA'
Takriban maafisa saba wa polisi wameuawa na 17 hawajulikani walipo baada ya kutokea shambulio nchini Kenya, ripoti zinasema.
Maafisa hao walivamiwa ghafla na watu wa kabila moja katika kaunti ya Turkana wakati wa shughuli za ulinzi siku ya Ijumaa.
Maafisa ambao hawajulikani walipo ni polisi wa akiba. Gazeti la Standard limesema helikopta ya jeshi imepelekwa kuwasaka.
Turkana, uliopo kaskazini mwa nchi hiyo, ni kaunti maskini kuliko zote Kenya na ni ya pili kwa ukubwa nchini humo.
Vyanzo ndani ya jeshi la polisi vimeiambia redio ya Kenya, Capital FM kuwa “bado hali ni tete” na jenerali inspekta wa polisi ameambiwa asizuru eneo hilo.
Wiki iliyopita magazeti ya Kenya yaliripoti kuwa watu watano, wakiwemo maafisa polisi, waliuawa karibu na eneo la tukio hili la Ijumaa lilipotokea.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment