Friday, 28 November 2014
UCHAGUZI WA KWANZA KWA ELEKTRONIKI AFRIKA
Raia wa Namibia leo wanachagua rais na wabunge – kwa kile kinachojulikana kuwa ni nchi ya kwanza kupiga kura kwa njia ya elektroniki barani Afrika.
Chama tawala cha South West Africa People's Organisation (Swapo) kinatarajiwa kushinda uchaguzi huo na waziri mkuu Hage Geingob kuwa rais.
Vyama vya upinzani vimekosoa mashine hizo za elektroniki zilizotengenezwa India, na kuonyesha wasiwasi kuwa upungufu wa karatasi unaweza kuchochea wizi wa kura.
Lakini kesi hiyo ilitupiliwa mbali na mahakama kuu wiki hii.
Takriban wapiga kura milioni 1.2 wana uwezo wa kupiga kura katika takriban vituo 4,000 vya kupiga kura nchini humo.
Maafisa kwenye vituo vya upigaji kura watathibitisha kadi ya upigaji kura katika kifaa cha taifa kilicho na taarifa za wapiga kura.
Katika chumba cha kupigia kura, mpigaji kura huchagua chama anachotaka kwa kubonyeza kitufye kwenye chombo maalum cha elektroniki.
Maafisa wa uchaguzi wanaamini matokeo yatatolewa saa 24 baada ya upigaji kura kumalizika.
Vyama 16 vinagombea nafasi za ubunge na wagombea wa urais ni tisa.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment