Sunday, 14 September 2014

'ABAKWA HADI KUFA' NA WAKE ZAKE 5



 sex1
Mfanyabiashara mwenye uwezo mkubwa na mwenye wake sita- amefariki dunia baada ya kile kinachodaiwa kulazimishwa kufanya mapenzi kwa mkupuo na wake zake wenye ‘wivu’.

Uroko Unoja, raia wa Nigeria alikuwa akifanya mapenzi na mke mdogo ambapo inaripotiwa wake waliobaki wakamvamia na visu na fimbo – kutaka afanye nao mapenzi pia.

Bw Onojo akafanya mapenzi na wake zake wanne mmoja baada ya mwengine, lakini akaacha kupumua baada ya mke wa tano kuelekea kupata zamu yake, kulingana na gazeti la Daily Post la Nigeria.

Wanawake wawili wamekamatwa kufuatia tukio hilo katika jimbo la Benue wiki iliyopita, ilisema ripoti hiyo, ikitumia sentensi ‘kubakwa hadi kufa’ kuelezea hatma ya mfanyabiashara huyo.





Bw Onoja inaaminiwa alikuwa karejea kutoka baa kwenye jumuiya ndogo ya Ugbugbu, Ogbadibo, kwenye saa tisa alfajir na kuelekea nyumbani kwa mke mdogo.

Wake zake wengine watano – ambao inasemekana walikuwa na mkutano wa kujadili hatua ya kuchukua kabla mume wao kurejea –  inadaiwa wakavamia chumba hicho wakiwa na visu na fimbo wakisistiza nao wapewe haki zao.
                                           
Inasemekana mfanyabiashara huyo mwanzo alikataa matakwa ya wake zake hao mpaka alipozidiwa nguvu.
Mke wake mdogo alinukuliwa akisema wenzake wengine watano walikimbilia msituni walipogundua mume wao amekufa.

Mkuu wa kijiji hicho, Okpe Odoh, aliiambia Daily Post kuwa suala hili limeripotiwa kwa polisi.


1 comment: