Majeshi ya Umoja wa Afrika ambayo tayari yapo yataanza kuvaa kofia za bluu |
Umoja wa Mataifa unachukua udhibiti rasmi wa shughuli za usalama za Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, ambapo takriban 25% ya watu eneo hilo wamekimbia makazi yao.
Hakuna majeshi mapya yaliyosambazwa kuongeza majeshi 5000 ya Afrika na 2,000 ya Ufaransa ambayo tayari yalikuwepo.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema majeshi zaidi yanahitajika haraka iwezekanavyo kumaliza ghasia hizo.
CAR imekuwa katika mgogoro tangu kundi la waasi lenye Waislamu wengi zaidi lilipochukua madaraka kwenye nchi yenye Wakristo wengi Machi 2013.
Kiongozi wa waasi Michel Djotodia alijiuzulu mwezi Januari baada ya shinikizo kubwa la kidiplomasia lakini mauaji yameendelea.
Waislamu wamekimbia mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi yao, huku nchi hiyo ikiwa imegawanyika Waislamu wakiwa kaskazini na Wakristo wakiwa kusini.
No comments:
Post a Comment