URAIA pacha kwa Watanzania walioko nje ya nchi
jana uliendelea kutawala katika mijadala kwenye Bunge la Katiba huku
wengi waliochangia wakikubaliana wasio na uraia Katiba iruhusu wapewe
chini ya utaratibu wa uraia wa pacha.
Wachangiaji wengi walisema hakuna sababu ya kuwanyima uraia hao kwa kisingizio kuwa sio wazalendo.
Selemani Ali alisema Watanzania walioenda nje ya nchi kusaka maisha
umefika wakati warejeshewe uraia wao kwani watapata fursa pia ya
kufaidika na matunda ya nchi yao.
Lakini Luis Majaliwa alisema Watanzania hao hawana hadhi ya kupewa
uraia kwa sababu si wazalendo kwani walikimbia nchi kwa kuona maisha ni
magumu na kuwaacha wenzao wanahangaika kuikwamua nchi kwenye maendeleo.
Alisema, “iweje leo hii walioacha jahazi linazama waona mambo yanaenda vizuri waruhusiwe kuja kupewa tena uraia.”

Alipendekeza Katiba isiwape hadhi ya kupewa uraia. Mjumbe Nyambali
Nyangwine alisema Katiba isiweke masharti magumu kwa Watanzania walioko
nje ambao wanataka kupata uraia wa nchini.
Alisema umefika wakati wa Watanzania kubadilisha fikra na msimamo na mitizamo yao dhidi ya Watanzania walioko nje ya nchi.
Zakia Meghji alisema walioko nje ya nchi ni Watanzania na wanafanya
kazi na sehemu ya fedha hizo wanazituma kwa jamii zao zilizoko nchini
na wanaweza kuja kuwekeza pia nchini.
Alisema hakuna sababu ya kuwakatalia kuwapa uraia kwani walikana
uraia wa hapa nchini ili waweze kufaidika na elimu ya nje pamoja kupata
ajira. “Hapa tunatoa uraia kwa watu ambao siyo Watanzania, iweje
tuwanyime watoto wetu uraia?” Alihoji Meghji.
Mussa Azzan Zungu alisema haoni sababu inayokera Watanzania hadi wawanyime Watanzania wenzao walioko nje kupatiwa uraia.
Hoja hiyo pia iliungwa mkono na Jasson Rweikiza ambaye alisema
umefika wakati watu waachwe wawe na uraia wa nchi mbili ili kutoa fursa
zaidi kwa vijana wa kitanzania kwenda nje kusaka maisha.
Ave Maria Semakafu alisema Watanzania hao walioko nje walienda huko
kusaka ajira kutokana na tatizo la ajira lililoko hapa nchini na
akahoji wakirudi wote hao ajira zitapatikana wapi? Alishauri mfumo wa
kuwapatia uraia ukubaliwe kwani kwenda kwao nje ya nchi sio kwamba
walikosa uzalendo ila walienda kusaka maisha zaidi.
Zainabu Gama naye alikubaliana na hoja hiyo na akasema kwamba kuwanyima uraia Watanzania hao ni kuwaonea.
Chanzo: Habarileo.co.tz
Chanzo: Habarileo.co.tz
No comments:
Post a Comment