Thursday, 11 September 2014

MTANZANIA ACHAGULIWA MAKAMU RAIS WA BET NETWORK




BET Networks, shina la Viacom Inc. (NASDAQ: VIA, VIAB), imetangaza kumwajiri Kay Madati kuwa Makamu wa Rais na Afisa Mkuu wa Digitali.

Madati, raia wa Tanzania aliyeishi Afrika, Uingereza na Marekani, ataiongoza timu nzima ya BET katika nyanya zote za kidigitali, mchakato wa masuala ya simu na mitandao ya kijamii na pia kusimamia shughuli zote za ubunifu, teknolojia na maendeleo katika mfumo mzima wa BET hasa unaohusika na masuala ya kidigitali.

Kabla ya kuteuliwa huko BET, hivi karibuni Madati alikuwa Mkuu wa Burudani na Habari Facebook Inc.

Yeye na timu yake walisaidia kuifanya Facebook Inc. kuwa mshirika mkuu upande wa kidigitali na kwenye mitandao ya kijamii kwa kushirikiana na studio za filamu, mifumo ya televisheni na makampuni ya burudani.

Kabla ya kujiunga na kampuni hiyo mwaka 2011, Madati alikuwa Makamu Rais wa kutathmini tabia za watazamaji/wasikilizaji kwa kupata habari CNN Worldwide na pia aliwahi kufanya kazi upande wa masoko Octagon Worldwide na BMW ya Amerika Kaskazini.




Chanzo: www.forbes.com

No comments:

Post a Comment