Monday, 15 September 2014

WAAFRIKA WATUMIA TAKRIBAN $7 BIL. KWA NYWELE BANDIA

 
Licha ya raslimali ndogo za fedha, Waafrika wanatumia takriban dola za kimarekani bilioni 7 kwenye nywele.

Kulingana na shirika la utafiti la kimataifa la Euromonitor, watu wa Afrika kusini, Nigeria na Cameroon pekee wanatumia takriban dola bilioni 1.1 kwenye bidhaa za nywele.

Hiyo ni pamoja na shampoo, mafuta ya nywele (lotion) na relaxer.

Kiwango cha pesa kinachopatikana kwa nywele bandia inazidi hata mafuta hayo ya nywele.

Inaripotiwa, faida inayopatikana kwa biashara ya nywele za kuongezea (weaves, wigs na extensions) ni takriban dola bilioni 6 kwa mwaka.

Biashara hiyo ya nywele barani Afrika imekua kiasi ambacho Unilever mjini Johannesburg inajitapa hasa.

L’Oreal nayo inafanya utafiti zaidi kwenye nywele za Kiafrika na ngozi ili kuongeza bidhaa zake za Dark And Lovely na nyinginezo.

"Ukuaji huu umetokea miaka 10 tu iliyopita, wanawake wana uthubutu inapokuja mitindo ya nywele", kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa L’Oreal Afrika Kusini.

Alisema ghafla sasa unaweza kutumia vifaa vya nywele ambavyo havikuwepo kabisa au vilikuwa ghali mno.

Nywele nyingi zinaouzwa barani Afrika hutoka Asia na hutengenezwa kwa bidhaa rahisi zaidi.


Nywele asili huuzwa pia, lakini hugharimu zaidi.

Chanzo: Africafrique.com
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment