Wednesday, 10 September 2014

MIFUPA YA DINOSARIA YAPATIKANA TANZANIA

Aina mpya ya Dinosaria (Dinosaurs)  imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania.

Mabaki hayo ya Dinosaria yaliyopewa jina la – ‘Rukwatitan Bisepultus’ – yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa, kusini magharibi mwa nchi hiyo.

baadhi ya mifupa ya  mnyama huyo iliyopatikana huko mkoani Rukwa
Baadhi ya mifupa ya mnyama huyo iliyopatikana huko mkoani Rukwa
Baadhi ya mifupa ya mnyama huyo iliyopatikana huko mkoani Rukwa

Inadhaniwa mnyama huyo aliyekuwa akiishi kwa kula majani, aliishi karibu miaka  milioni 100 iliyopita, na alikuwa na uzito sawa na tembo kadhaa na alikuwa na miguu ya mbele yenye urefu wa mita mbili.

Mnyama huyo ni aina ya Titanosaurus ambao ni wakubwa, na wanaokula nyasi.

Gorscak etal_Fig 3_Silhouette

Mabaki ya wanyama aina hiyo mpaka sasa yamepatikana katika maeneo ya Amerika ya Kusini, bara ambalo lilijitenga kutoka Afrika katika kipindi cha Cretaceous, (kipindi ambacho miamba ya chokaa iliumbika) takriban miaka milioni 140 iliyopita.

Eneo la bonde yalikopatikana mabaki ya mnyama huyo mkubwa. Picha kwa hisani ya Patrick O’Connor wa Ohio University

Tanzania ina historia ya kuwa na wanyama hao wakubwa.Mwaka 1906 wanasayansi kutoka Ujerumani waligundua mabaki ya dinosaria kule Tendaguru, Lindi, wakayafukua na kuyapeleka Ujerumani ambako yamehifadhiwa tangu wakati huo.

Je, mifupa hiyo iliyogundulika Rukwa itabaki Tanzania iwe kivutio cha utalii na utafiti au itatoka nje ya nchi?

Chanzo: taarifa.co.tz

No comments:

Post a Comment