Muigizaji Richard Kiel - aliyecheza kama mwovu mwenye meno ya bati maarufu kama Jaws katika filamu za James Bond - amefariki dunia California akiwa na umri wa miaka 74.
Msanii huyo maarufu wa Marekani, aliyeigiza kwenye filamu ya The Spy Who Loved
Me mwaka 1977 na Moonraker mwaka 1979,aliaga dunia katika hospitali ya Fresno siku ya Jumatano.
Msemaji wa Kituo cha Matibabu cha Saint Agnes amethibitisha kifo cha Kieli, lakini hakusema sababu.
Muigizaji huyo mwenye urefu wa mita 2.18 pia aliigiza kwenye filamu ya vichekesho ya Happy Gilmore, ambapo muigizaji mkuu alikuwa Adam Sandler mwaka 1996.
Alipata umaarufu sana kwa jina la Jaws akiigiza na Roger Moore mwenye jina la 007.
Sir Roger alisema "amehuzunishwa mno" kutokana na kifo cha muigizaji mwenzake.
"Tulikuwa pamoja kwenye kipindi kimoja cha redio wiki moja tu iliyopita," alisema muigizaji huyo maarufu wa Bond, akiongeza "siwezi kuhimili taarifa hii".
No comments:
Post a Comment