Thursday, 11 September 2014

BILL GATES ATOA FEDHA KUPAMBANA NA EBOLA



 Liberian health care workers on an Ebola burial team collect the body of an Ebola victim at a motor vehicle garage in Paynesville on the outskirts of Monrovia, Liberia (9 September 2014)
Fedha zaidi zimetangazwa kusaidia dharura iliyopo kusaidia katika kupambana na mlipuko wa Ebola, Afrika magharibi.

Wakfu wa Bill Gates inatoa dola za kimarekani milioni 50 kusaidia jitihada za kupambana na kirusi hatari kwenye nchi zilizoathirika.

Msaada huu unatolewa kuongezea fedha nyingine zilizotangazwa na serikali za Uingereza na Marekani, pamoja na Umoja wa Ulaya.

Lakini baadhi ya mashirika ya kutoa misaada ilisema kinachohitajika zaidi na haraka barani Afrika ni wataalam wa kuweza kuzuia kusambaa kwa maradhi hayo.

Wakfu wa Gates – ulioundwa na muasisi wa Microsoft Bill Gates na mkewe Melinda imesema itatoa haraka iwezekanavyo “fedha zinazohitajika” kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika mengine yanayohusika na mpambano dhidi ya Ebola, ili kununua vifaa vinavyotakiwa.

Na imesema itafanya kazi bega kwa bega na washirika wengine kuharakisha utengenezaji wa dawa na chanjo dhidi ya virusi hivyo, ambavyo vimesababisha takriban vifo vya watu 2,300.

No comments:

Post a Comment