Saturday 13 September 2014

UGANDA YATAHADHARISHWA JUU YA AL-SHABAB

Uganda's Entebbe Airport on 3 July 2014
Usalama uliimarishwa maeneo muhimu, ukiwemo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe

Serikali ya Uganda imegundua chumba cha magaidi inachoamini walikuwa wakijiandaa kufanya shambulio wakati wowote, ubalozi wa Marekani mjini Kampala ulisema.

Ubalozi huo umesema chumba hicho kinamilikiwa na kundi la Somalia la Al- Shabab, lakini hilo bado linatakiwa kuthibitishwa na polisi wa Uganda.

Awali ubalozi huo uliwaonya raia wa Marekani kubaki nyumbani wakati wa harakati za polisi za kukisaka chumba hicho.

Polisi Uganda walisema wameimarisha usalama kwenye maeneo ya umma mjini Kampala, na kukamata watu kadhaa.

Mapema wiki hii, ubalozi wa Marekani ulionya uwezekano wa kuwepo mashambulio ya kulipiza kisasi dhidi ya Wamarekani yatakayofanywa na al-Shabab kufuatia shambulio la anga lililomwuua kiongozi wao Ahmed Abdi Godane, Septemba 2.

Washukiwa wanaaminiwa kuwa raia wa kigeni, amesema mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga.

Kundi hilo la al-Shabab, linalotaka kupindua serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa limemtaja Ahmad Umar kuwa kiongozi wao mpya.







No comments:

Post a Comment