Tuesday, 9 September 2014

SAFARI ZIENDELEE LICHA YA EBOLA KUSAMBAA - AU



 

Wakuu wa Umoja wa Afrika wametoa wito wa kuondolewa kwa vizuizi vya safari vilivyotolewa kwenye nchi zilizoathirika na maradhi ya Ebola licha ya shirika la Afya Duniani WHO kuonya maelfu ya watu wengine kuathirika katika wiki chache zijazo.

“Nchi wanachama wafute vizuizi vyote vya safari ili kufungua fursa za kiuchumi,” Mkuu wa tume ya AU Nkosazana Dlamini-Zuma aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa dharura mjini Addis Ababa, Ethiopia, ulioitishwa kujadili kuhusu Ebola.

Lakini alisema “lazima mchakato thabit wa kupima uwekwe”.

Idadi ya waliofariki dunia kutokana na maradhi hayo ya Ebola – yanayoenea Afrika magharibi, huku Liberia, Guinea na Sierra Leone zikiwa zimeathirika zaidi, imefikia 2,000, huku takriban 4,000 sasa wakiwa wameambukizwa, WHO imesema.

Shirika la Umoja wa Mataifa limeionya Liberia kuwa “maelfu” ya maambukizi mapya ya Ebola yataibuka katika kipindi cha wiki tatu zijazo, ongezeko kubwa sana kutoka idadi ya 2,000 walioathirika sasa.

Katika harakati za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo, baadhi ya nchi zilizoathirika zimezuia eneo zima watu kutoka, wakati baadhi ambao hawajaathirika wamesimamisha safari za ndege.

 Wataalamu wameonya kutetereka kwa uchumi ambapo kumesababishwa na vizuizi hivyo vinaongeza madhila kwenye bara hilo la Afrika, wengine wakisema kuzuia safari za ndege kumepunguza kasi ya kupeleka tiba maeneo yaliyoathirika.

Chanzo: Al Jazeera                                   
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment