|
Jerome Champagne ametangaza nia ya kupambana na Sepp Blatter katika kuwania urais wa Fifa |
Jerome Champagne ametangaza nia ya kupambana na Sepp Blatter katika kuwania urais wa Fifa.
Raia wa Ufaransa Jerome Champagne amethibitisha mipango yake kupambana na Sepp Blatter kwa ajili ya urais wa Fifa.
Blatter alitangaza nia yake ya kuwania muhula wa tano wiki iliyopita.
Mwanadiplomasia Champagne, 56, alifanya kazi Fifa kwa miaka 11 kama mkurugenzi kabla ya kuondoka 2010.
“Nimeshawaandikia Kamati ya Uchaguzi ya Fifa na rais wake, Bw
Domenico Scala, kuthibitisha nia yangu ya kugombea urais wa Fifa,”
aliandika mtandaoni.
Champagne anahitaji msaada wa wanachama watano wa Vyama vya Soka wa
Fifa ila hawezi kutangaza ni wa kina nani mpaka tangazo rasmi
litakapotolewa mwezi Januari.
Uchaguzi utafanyika kwenye mkutano wa Fifa mwezi Juni mwakani.
Chanzo: taarifa.co.tz
No comments:
Post a Comment