Kuna wasiwasi hatua ya serikali hiyo itavuruga jitihada za kupambana na ukosefu wa chakula |
Serikali ya Sudan kusini imetoa amri kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na makampuni binafsi kuwafukuza baadhi ya wafanyakazi wa kigeni ifikapo mwezi Oktoba.
Wizara ya kazi imesema kazi kama za mapokezi hadi wakurugenzi katika siku za usoni zifanywe na raia wa Sudan kusini.
Shirika la kutoa misaada la Oxfam limesema hatua hiyo itakuwa na athari kubwa kwenye miradi hiyo ya misaada.
Takriban watu milioni mbili wamekimbia makazi yao tangu makundi mawili hasimu wa chama tawala kupigana mwezi Desemba.
Maelfu ya watu wamekufa kwenye mapambano hayo na mashirika ya kutoa misaada yamesema hadi watu milioni nne wako katika hatari ya kukosa chakula kutokana na mgogoro huo.
Kilichoanza kama ugomvi wa kisiasa baina ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa naibu wake Riek Machar uligeuka kuwa mapigano ya kikabila.
No comments:
Post a Comment