Monday, 22 September 2014

ETIHAD YAANZA SAFARI ZA DAR ES SALAAM





Etihad Airways, ndege ya taifa ya UAE itapanua safari zake za barani Afrika kwa kuanzisha safari za kila siku mjini Dar es Salaam, mji mkubwa kuliko wote Tanzania.

Safari za ndege baina ya Abu Dhabi na Dar es Salaam, zitakazoanza tarehe 1 Desemba 2015, zitafanyika kutumia ndega aina ya Airbus A230 ikiwa na viti 16 vya daraja ya Business na viti 120 vya daraja ya Economy.

Dar es Salaam itakuwa nchi ya 110 duniani kufikiwa na Etihad Airways, na nchi ya 11 barani Afrika na eneo la Bahari ya Hindi.

Safari hiyo ya kila siku itapitia Abu Dhabi, na safari za kuunganisha kwenda mataifa maarufu 45 kupitia  Mashariki ya Kati, Ulaya, maeneo ya kusini mwa India, Kaskazini na kusini-mashariki mwa Asia na Australasia.

Matumaini makubwa ni kuwa njia hizo mpya za safari zitaongezwa nguvu na wasafiri wengi wanaofanya biashara na waendao likizo, pamoja na ukubwa wa mizigo, kati ya maeneo ya Afrika Mashariki, maeneo ya kusini mwa India pamoja na China.

No comments:

Post a Comment