Wednesday, 17 September 2014

CHUO CHA NIGERIA CHASHAMBULIWA

Security officers stand guard at the campus of Kano State Polytechnic on 30 July
Milio ya risasi na mlipuko umesikika katika chuo cha walimu cha mafunzo kwenye mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria.
Wanafunzi walionekana wakikimbia kutoka chuo hicho.
Mwanafunzi mmoja aliiambia BBC kuwa aliona miili 17 katika eneo hilo.
Haiko wazi nani anahusika na shambulio hilo, japokuwa hisia zitaelekea kwa kundi la Boko Haram, ambalo limekuwa likifanya mashambulio Nigeria tangu mwaka 2009.
Mwezi Julai mji huo ulikumbwa na mashambulio matano katika kipindi cha siku nne, moja likiwa limelengwa kwenye chuo kingine na kuua sita.
Mwezi Mei 2013, Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika majimbo ya kusini ya Borno, Yobe na Adamawa, akiahidi kuwamaliza wapiganaji hao.
Hatahivyo wapiganaji hao wameongeza mashambulio, na kuua zaidi ya raia 2,000 mwaka huu, kulingana na shirika la kutetea haki za binadamu HRW.

No comments:

Post a Comment