Thursday, 25 September 2014
ASAMOAH GYAN AKANA KUMTOA RAFIKI YAKE 'KAFARA'
Kapteni wa Ghana Asamoah Gyan alisema madai kuwa alimwuua rafiki yake ambaye ni msanii wa miondoko ya hip-hop Castro kama sehemu ya kafara ni “ upuuzi mtupu”.
Msanii Castro, ambaye jina lake halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka , pamoja na rafiki yake Janet Bandu,mwezi Julai.
Walitoweka walipoenda likizo na familia ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Sunderland , Gyan katika mji wa Ada kwenye pwani ya Ghana.
Madai yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Ghana vinasema kutoweka huko kunaonyesha mazingira ya utata.
Castro na Bandu mara ya mwisho walionekana wakielekea kwenye pwani hiyo kwenye motokari ya majini ‘jet ski’ na baadae kutangazwa kuwa walizama.
Hakuna miili yoyote iliyoopolewa mpaka sasa na uvumi uliendelea kusambazwa mwezi huu baada ya kaka yake, Baffour Gyan, akidaiwa kuwa sehemu ya genge lililomshambulia mwandishi wa habari aliyemhoji mchezaji huyo kuhusu uvumi huo.
Kwa sasa hata hivyo, Baffour Gyan amefutiwa makosa yake.
Hisia hizo zilisababisha Gyan mwenye umri wa miaka 28 aliyejiunga na Al-Ain ya UAE mwaka 2011, kufanya mkutano na waandishi wa habari.
Wakili wake Kissi Agyabeng alisema familia yake imepata "mshtuko" na wamebaki kimya mpaka sasa kwa kuwa hawakutaka kuingilia uchunguzi wa polisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment