Pendekezo la Mahakama Kuu ya Madras kuwataka wanaume na wanawake kufanya
vipimo kabla ya kufunga ndoa limewafurahisha wengi huko kusini mwa India na la
kushangaza wanawake wengi wameridhishwa na uamuzi huo kuliko wanaume.
"Watoto wa kike mpaka leo wanaonekana kama mzigo usio na umuhimu. Bila hata
uchunguzi wa kutosha wa bwana harusi, binti hutolewa kwenye familia zao kwa minajil ya
ndoa," Justice N Kirubakaran
ameshuhudia katika kesi moja ambapo mwanamke anadai talaka kwa madai kuwa mumewe
hana nguvu za kiume.
Uamuzi huo wa mahakama pia umewafurahisha wanasheria, watabibu na jumuiya
ya wanafunzi.
Mwanasheria T S R
Venkataramana alisema, “Pendekezo la mahakama ni sahihi na ni mabadiliko
chanya. Lakini katika hali ya uhalisia haliwezekani. Jamii yetu lazima ibadilike kulikubali hilo.”
Dr Abdul Latiff alisema,
“Siku hizi, watoto wa kike na wa kiume wana taarifa nyingi za ngono, ambazo
wanajifunza kupitia televisheni na mtandao. Hivyo vipimo kabla ya ndoa ni jambo
jema.
Hata hivyo, alisema si rahisi kutekeleza. Miaka
kadhaa iliyopita, kuonyesha cheti cha hospitali cha kupima ukimwi kabla ya ndoa
ilisistizwa, hata hivyo, lengo halikufanikiwa.
Chanzo: The Times of India
kweli ni bora kujua nini na vipi ndoa yenu itakavyokuwa
ReplyDelete