Thursday, 18 September 2014

MEYA WA TORONTO APATA SARATANI YA 'KIPEKEE'



Rob Ford
Bw Ford alilazwa hospitali siku ya Alhamis na kukutwa na uvimbe tumboni

Meya wa Toronto Rob Ford amekutwa na saratani ambayo ni nadra mtu kupata “na ni ya hatari ”, madaktari wanaomtibu wamesema.
.
Bw Ford, mwenye umri wa miaka 45, ana saratani inayoweza kusambaa haraka kwenye tumbo lake

Anatarajia kuanza matibabu ya mionzi katika kipindi cha saa 48 zijazo.

Ana uvimbe wa sentimeta 12 kwa 12 kwenye tumbo na nyingine ndogo yenye sentimeta 2 kwenye tako lake la kushoto, ambapo inaaminiwa kukua katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

“Nina matumaini makubwa kuhusu tiba hii,” alisema Dk Zane Cohen, ambaye anasimamia timu nzima inayomshughulikia meya huyo.

Bw Ford alijiengua kwenye kampeni za uchaguzi mpya baada ya kupatikana na uvimbe wa tumbo.

Meya huyo mwenye utata, aliyekiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine akiwa bado madarakani, bado ana wafuasi wengi licha ya wito wa kutaka ajiuzulu.

Pia aliwahi kuchukuliwa video akitishia kumwuua mtu asiyejulikana, na pia kutoa kauli chafu za ngono kwa waandishi wa habari.



No comments:

Post a Comment