Wednesday, 17 September 2014
DAKIKA ZA MWISHO ZA KAMPENI USKOCHI
Pande zote mbili katika mjadala juu ya kura za maoni za Uskochi wako katika dakika za lala salama kuwashawishi wapiga kura ikiwa ni siku ya mwisho ya kampeni.
Haya yanatokea huku matokeo ya maoni yaliyotolewa hivi karibuni yanaonyesha kura hizo zinakaribiana sana, ambapo kura ya “Hapana” (wasitengane) inaongoza kwa kiwango kidogo sana.
Waziri kiongozi wa Uskochi Alex Salmond amewaandikia wapiga kura akiwataka wapige kura ya “Ndio”, akisema “wakati ndio huu”.
Wanaoongoza kampeni ya kuunga mkono muungano waitwao ‘Better Together’ walikesha kuwasahaiwshi wale wanaofanya kazi usiku, huku wale wanaopinga wakiwa na kauli mbiu ya “Love Scotland”.
Maoni mengine yaliyochapishwa na magazeti matatu, siku ya Jumanne, huku wale ambao hawajaamua bado kuchagua upande upi, yote yameonyesha kura ya “Hapana” inaongoza kwa 52% kwa 48%.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment