Jenerali Nyamwasa ameilaumu serikali ya Rwanda kuhusika na ufyatuliaji risasi |
Mahakama
ya Afrika kusini imewahukumu watu wanne kufungwa miaka nane jela kwa kosa la
jaribio la kumwuua aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Faustin Kayumba
Nyamwasa.
Alipigwa
risasi tumboni mjini Johannesburg Juni 2010, siku chache baada ya kukimbia
Rwanda baada ya mfarakano na Rais Paul Kagame.
Hakimu mkazi alisema “watuhumiwa wakuu” hawajakamatwa.
Mashambulio kadhaa dhidi ya waombaji hifadhi wa Rwanda nchini Afrika kusini yamesababaisha mvutano wa kidiplomasia baina ya Pretoria na Kigali.
Serikali ya Rwanda imekana kabisa kuhusika na mauaji ya wapinzani wake Afrika Kusini.
'Bado wana woga '
Upande wa mwendesha mashtaka ulitaka wapewe kifungo cha
miaka 15 kwa Wanyarwanda wawili, Amani Uriwane na Sady Abdou, na Watanzania wawili
Hassan Mohammedi Nduli na Hemedi Dendengo Sefu,waliotiwa hatiani kwa jaribio la
mauaji.
Kuwapa kifungo cha miaka minane kila mmoja, Hakimu Stanley Mkhari alisema kuwa watu hao walikuwa kizuizini tangu tukio hilo la ufyatuaji risasi kutokea.
"Nyie si watuhumiwa wakuu katika suala hili. Kwa maoni yangu mlitakiwa kuwa mbele yangu na wote waliowezesha pesa kupatikana na waliowafadhili kufanya uhalifu huo," amenukuliwa akisema.
Wanaume wengine wawili waliachiwa huru kwa kuhusishwa na
kosa hilo mwezi uliopita.
Jenerali Nyamwasa alisema alikuwa amefurahi baada ya kutolewa
uamuzi wa hukumu hiyo, lakini bado ana wasiwasi na usalama wa Wanyarwanda
waishio uhamishoni, shirika la habari la Reuters limesema.
No comments:
Post a Comment