Bi Wanpen alijirusha kwenye eneo hili la kuhifadhia mamba Samut Prakarn |
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 65 kutoka Bangkok amejiua kwa kujirusha kwenye kundi la mamba eneo wanalofugwa karibu na mji mkuu, polisi walisema.
Walioshuhudia walimwona Wanpen Inyai akijirusha kwenye dimbwi la mamba hao, gazeti la Bangkok Post liliripoti.
Wafanyakazi wa eneo hilo walishindwa kumwokoa.
Polisi walisema waliambiwa na familia yake kuwa Bi Wanpen alionekana mwenye msongo wa mawazo kabla ya kifo chake.
Vivutio vya kitalii vya Thai inasemwa aghalabu huwa na sheria kali za kiusalama.
Kulingana na ripoti iliyotolewa, alivua viatu vyake kabla ya kujirusha katikati ya bwawa hilo lenye kina cha mita 3 lililo na mamia ya mamba.
Wafanyakazi wa eneo hilo la kitalii walijaribu kutumia fimbo ndefu kuzuia mamba hao kumshambulia mama huyo, kulingana na Bangkok Post.
Mapema siku hiyo, familia ya Bi Wanpen ilijaribu kuripoti kuwa hajulikani alipo baada ya kuona alitoweka, lakini waliambiwa wasubiri hadi saa 24.
Kifo kama hicho kiliwahi kutokea mwaka 2002 katika eneo hilohilo, na mwengine pia alijiua hapohapo muongo mmoja uliopita.
No comments:
Post a Comment