Sunday, 28 September 2014
NYOTA WA FILAMU GEORGE CLOONEY AFUNGA NDOA
Nyota muigizaji wa Hollywood George Clooney amemwoa mwanasheria wa kutetea haki za binadamu Amal Alamuddin huko Venice, miongoni mwa matukio yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu zote.
Wenzake ambao ni maarufu pia kwenye tasnia ya uigizaji na uimbaji katika mji wa Italia walimiminika kushuhudia muungano huo wa kapera maarufu katika uwanda wa filamu, mwenye umri wa miaka 53, na Bi Alamuddin, mwenye umri wa miaka 36.
Shughuli hiyo ilisherehekewa katika hoteli iliyoelekea kwenye mfereji mkubwa wa Venice.
Wakala wa Clooney walitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari.
Kulingana na shirika la habari la AP, hiyo ndio itakuwa taarifa pekee itakayotolewa kuhusu harusi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment