Tuesday 9 September 2014

MAJESHI YA AU 'YABAKA' MABINTI SOMALIA

 

Majeshi ya Umoja wa Afrika AU yanayodhaminiwa na mataifa ya kigeni yaliyopo Somalia yamewabaka kwa pamoja wanawake na watoto wa kike, wengine, mpaka wakiwa chini ya umri wa miaka 12 na kutumia chakula cha misaada kama biashara ya kupata ngono, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, HRW limesema.

Majeshi 22,000 ya AU, yanayoitwa AMISOM, yakiwa na wanajeshi kutoka mataifa sita, yamekuwa yakipigana sambamba na majeshi ya serikali dhidi ya kundi linalohusishwa na al-Qaeda la al-Shabab tangu mwaka 2007.

"Baadhi ya wanawake waliobakwa walisema wanajeshi hao huwapa chakula au pesa baada ya kitendo hicho katika jaribio la kutoa madai ya kufanya ngono kwa makubaliano," HRW imesema kwenye ripoti hiyo.

AMISOM imesema madai hayo ya ubakaji ni"ya nadra" na kuita ripoti hiyo "kutokuwa na uwiano na inapendelea".

Wafadhili wa AMISOM ni Umoja wa Ulaya na Marekani

Chanzo: Al Jazeera
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment