Thursday, 25 September 2014

"MBU WAZURI" KUPAMBANA NA DENGE - BRAZIL

Watafiti wa Brazil mjini Rio de Janeiro wamewatawanya maelfu ya mbu walio na bakteria anayefubaza homa ya dengu.

Matumaini ni kuwa watazaliana, na kuongezeka kwa wingi, hivyo kupunguza watu wanaopata ugonjwa huo.

Mchakato huo ni sehemu ya mradi unaofanyika pia Australia, Vietnam na Indonesia.

Bakteria huyo, Wolbachia, hawezi kuingiziwa kwa binadamu

Mradi huo ulianza mwaka 2012 alisema Luciano Moreira wa taasisi ya utafiti ya Brazil iitwayo Fiocruz, ambaye ndiye anasimamia utafiti huo.

Alisema maelfu ya mbu hao wataachiwa wazunguke wanapotaka kila mwezi kwa muda wa miezi minne, mwanzo wakianzia Tubiacanga, kaskazini mwa Rio.

Bakteria "Wazuri'

Bakteria Wolbachia anapatikana kwenye wadudu kwa 60%. Hufanya kazi kama kinga kwa mbu anayehifadhi denge, Aedes aegypti, akizuia virusi vya dengu kuzaliana mwilini.

Wolbachia pia ana athari yake kwenye uzalishaji. Ikatokea mbu dume aliye na virusi hivyo akarutubisha mayai ya jike bila ya bakteria hao, mayai hayo hayaingii kwenye hatua ya lava.

Iwapo wote jike na dume wakiwa na virusi hivyo au kama jike tu ndio ana bakteria, vizazi vyote vya siku za usoni vya mbu hao watakuwa na Wolbachia.

Kwa matokeo hayo, mbu wa Aedes ambao wana Wolbachia wanakuwa wengi bila hata watafiti kuendelea kuwasambaza wadudu walioathirika kila mara . Maradhi ya dengu yaliibuka upya Brazil mwaka 1981 baada ya kutoweka kabisa kwa zaidi ya miaka 20.

Baada ya miaka 30 iliyofuata, watu milioni saba waliripotiwa kuathirika.

Brazil inaongoza duniani kwa idadi ya watu walioathirika na denge, huku wakiwepo watu milioni 3.2 walioathirika na 800 kufariki kutokana na ugonjwa huo baina ya mwaka 2009 - 2014.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu


No comments:

Post a Comment