Olga Raschietti amekaa miaka mingi Afrika ya Kati |
Polisi nchini Burundi imesema watawa watatu,
watu wazima wamebakwa na kuuawa kwenye makazi yao nje ya mji mkuu Bujumbura.
Watawa wawili waliuawa siku ya Jumapili huku
mtawa wa tatu ambaye mwili wake uligundulika mapema siku ya Jumatatu ulikutwa
kichwa chake kikiwa kimekatwa.
Watawa hao wametajwa kuwa Lucia Pulici, mwenye umri wa
miaka 75, Olga Raschietti, miaka 82, na Bernadetta Boggian, mwenye miaka 79.
Serikali imesema anayeshukiwa kufanya mauaji
hayo katika shambulio la kwanza alionekana akikikmbia makazi ya watawa hao huku
akiwa na kisu mkononi.
Dayosisi ya Italia huko Parma imesema watawa
hao wameuawa kukiwa na jaribio la ujambazi.
Hatahivyo, polisi wa Burundi, wamesema nia
yao haijulikani ni nini, kwani hakuna pesa zozote zilizoibiwa.
Mwaka 2011, mtawa kutoka Croatia na
mfanyakazi wa kutoa misaada wa Italia waliuawa katika jaribio la wizi kaskazini
mwa Burundi.
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment