Friday, 19 September 2014

MWANASIASA WA ZIMBABWE AFA KANISANI

 A rescue workers at the site of a collapsed building at the Synagogue Church of All Nations in the Ikotun-Egbe neighbourhood of Nigeria's commercial capital Lagos, 17 September 2014

Mwanasiasa wa Zimbabwe wa upande wa upinzani ni miongoni mwa watu 80 waliofariki dunia baada ya kanisa moja mjini Lagos, Nigeria kuporomoka wiki moja iliyopita.

Greenwich Ndanga alikuwa mwenyekiti kupitia chama cha Movement for Democratic Change (MDC) wa wilaya ya Mashonaland West.

Wengi waliofariki dunia kwenye tukio hilo ni raia wa Afrika kusini waliokuwa wakiishi kwenye jengo hilo lenye ghorofa kadhaa linalomilikiwa na kanisa la mhubiri maarufu TB Joshua.

Serikali ilisema ilikuwa na ghorofa nyingi kuliko ilivyoweza kuhimili.

Zaidi ya watu 130 walinusurika, akiwemo mwanamke mmoja wa Afrika kusini aliyetolewa kwenye kifusi siku ya Jumatatu - siku tatu baada ya jengo kuporomoka.

Kifo cha Bw Ndanga kilithibitishwa na familia yake na maafisa wa chama siku ya Alhamisi.

Msemaji wa MDC Douglas Mwonzora alisema Bw Ndanga alikuwa mchungaji na alikwenda Nigeria kwa shughuli za kanisa, limeripoti gazeti la taifa la Zimbabwe, Herald.


No comments:

Post a Comment