Saturday 15 November 2014

PADRI WA UGANDA AKUTWA KABURINI MEXICO



Mass grave in Pueblo Viejo, Mexico, 6 Oct 14

Wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi nchini Mexico wamegundua mwili wa mchungaji wa Kikatoliki kutoka Uganda, ikiwa ni  miongoni mwa mabaki ya miili iliyopatikana kwenye kaburi lenye watu wengi mwezi uliopita.

Mchungaji John Ssenyondo alikuwa hajulikani alipo tangu alipotekwa katika jimbo la Guerrero lililopo kusini-magharibi, miezi sita iliyopita.

Kaburi hilo liligunduliwa na polisi waliokuwa wakiwatafuta wanafunzi 43 ambao walitoweka eneo hilo tarehe 26 Septemba.

Tukio la kupotea au kutojulikana walipo wanafunzi hao wa ualimu lilisababisha hasira kali Mexico na kusababisha msako wa kitaifa.

Vipimo vya asidi nasaba (DNA) vilivyofanywa mapema mwezi huu vimeonyesha miili kwenye kaburi hilo lililojificha karibu na mji wa Ocotitlan – ambapo mabaki ya Mchungaji Ssenyondo yalipatikana – si ya wanafunzi hao.

Mchungaji Ssenyondo alitekwa Aprili 30 na watu wasiojulikana wenye silaha, ambao waliweka vizuizi barabarani na kumlazimisha kuingia kwenye gari lao.

Alikuwa nchini humo kwa miaka mitano. Vipimo vyake vya meno ndivyo vimesaidia kumtambua.

"Hatujui lengo lao,'' alisema Victor Aguilar, mwakilishi wa dayosisi ya Chilpancingo-Chilapa. "Unajua ukatili umeenea sana katika jimbo hili."

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

2 comments:

  1. haya maajabu kutoka uganda na kukuta mexco hii hatari na walimwengu wana malimwengu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haya bibie Allah akupe nguvu Blog hii ifike kote duniani kwakuwa na wasomaji wengi inshaallah1

      Delete