Friday, 21 November 2014
KENYA YACHUNGUZA 'WAFANYAKAZI HEWA' 12,000
Serikali ya Kenya imeamuru uchunguzi ufanyike baada ya zaidi ya majina ya uongo 12,000 kuwepo kwenye hati za malipo.
Majina hayo yaligunduliwa baada ya mamlaka kuanza kusajili wafanyakazi wote wa serikali mwezi Septemba kwa njia ya elektroniki.
Tume ya kupambana na rushwa ya Kenya na kitengo cha kupambana na udanganyifu katika mabenki zimeombwa na baraza la mawaziri kuanza uchunguzi.
Kenya imewekwa nafasi ya 136 kati ya mataifa 177 na shirika la kimataifa la Transparency kutokana na rushwa
Mapema mwaka huu uchunguzi wa kifedha uligundua takriban $1m (£600,000) kwa mwezi zilikuwa zinapotea kwa "wafanyakazi hewa", pamoja na mchanganyiko mwengine wa fedha.
Serikali ya nchi hiyo ina shuku kuwa waliokuwa wafanyakazi waliendelea kupokea mishahara hata baada ya kuacha kazi.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment