Tuesday, 11 November 2014

MSHTAKIWA WA MAUAJI YA MEWIYA AACHIWA HURU


Senzo Meyiwa during the CAF Champions League Final between Orlando Pirates and Al Ahly in Soweto, SA - 02 November 2013

Mahakama ya Afrika Kusini imefuta mashtaka ya mauaji dhidi ya mwanamme aliyehusishwa kumwuua kapteni wa soka wa taifa Senzo Meyiwa.

Zanokuhle Mbatha alikamatwa na timu maalum ya polisi mwezi uliopita baada ya msako wa kitaifa.

Hakimu aliamuru aachiwe huru kwasababu hapakuwa na ushahidi wa kutosha wa yeye kushtakiwa.

Meyiwa aliuawa kwenye tukio la ujambazi nyumbani kwa mpenzi wake kwenye kitongoji cha Vosloorus, mashariki mwa Johannesburg.

Wanaume wawili wanadaiwa kuingia nyumbani kwa Kelly Khumalo tarehe 26 Oktoba na kuwaamrisha watoe simu zao za mkononi kabla ya kumwuua Meyiwa wakati wa purukushani.

No comments:

Post a Comment