Thursday, 27 November 2014

PELE ALAZWA BRAZIL



 

Nyota wa soka wa Brazil Pele amehamishiwa katika idara maalum kufuatia kupata maambukizi kwenye njia ya haja ndogo.

Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo imesema nyota huyo mwenye umri wa miaka 74 aliyeshinda mara tatu kwenye kombe la Dunia amehamishwa baada ya “kuumwa mara kwa mara”.

Ripoti zilisema Pele, aliyelazwa siku ya Jumatatu, alikuwa katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi.

Pele, mshindi katika Kombe la Dunia mwaka 1958, 1962 na 1970, awali alitolewa hospitalini Novemba 13 baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa mawe kwenye figo.

Inaeleweka kwamba wakati huduma maalum ni zaidi ya huduma ya kawaida, lakini si hatari sana kama ilivyo kwenye chumba maalum cha wagonjwa mahututi, na Mbrazil huyo ambaye bado anaheshimika kama mchezaji wa kipekee kuwepo duniani – bado anaweza kutembelewa na wageni.


No comments:

Post a Comment