Friday 21 November 2014

BASI LA KWANZA KUTUMIA 'KINYESI CHA BINADAMU'



 Bio-Bus

Basi la kwanza la Uingereza linaloendeshwa kwa kutumia kinyesi cha binadamu na vyakula vibovu limeanza kazi baina ya Bristol na Bath.

Basi hilo lenye uwezo wa kuchukua watu  40 liitwalo "Bio-Bus" linatumia gesi ya  biomethane inayotokana na vyakula vibovu na maji taka pia.

Basi hilo linalozingatia masuala ya mazingira linaweza kusafiri hadi kilomita 300 katika tangi moja la gesi, linalochukua takriban kinyesi cha watu watano kuzalisha kwa mwaka.

Linaongozwa na Kampuni ya Basi ya Bath na litakuwa linasafiri kutoka uwanja wa ndege wa Bristol hadi katikati ya mji wa Bath.

Gesi hiyo ya biomethane inazalishwa katika kiwanda cha taka cha Bristol, inayoendeshwa na kampuni ya GENeco, ambayo ni tawi la Wessex Water.

Meneja wa GENeco Mohammed Saddiq alisema: "Magari yanayotumia gesi yana wajibu mkubwa wa kuimarisha hali bora ya hewa katika miji ya Uingereza lakini Bio-Bus linavuka mipaka zaidi na linapata nishati yake kutoka kwa watu wanaoishi eneo hilo, wakiwemo bila shaka wanaopanda basi hilo.”

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment