Tuesday 17 March 2015

WABUNGE WA UPINZANI 21 WAFUKUZWA ZIMBABWE


 Morgan Tsvangirai greeting supporters in Harare in 2014
Wabunge wa upinzani 21 wamefukuzwa kutoka bunge la Zimbabwe baada ya kujitoa na kuunda chama kipya.

Spika Jacob Mudenda aliagiza kufukuzwa kwa wabunge hao, wanaoongozwa na aliyekuwa waziri wa fedha Tendai Biti.

Kundi hilo liligombea uchaguzi wa mwaka 2013 chini ya Morgan Tsvangirai wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC).

Baadae wakagawanyika kuunda MDC mpya baada ya kukataa uongozi wake.

Kufukuzwa kunatoa fursa kwa uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya wabunge hao 14 ambao walichaguliwa moja kwa moja, aliripoti mwandishi wa habari wa BBC Brian Hungwe kutoka kutoka mji mkuu Harare.

No comments:

Post a Comment