Wednesday, 3 June 2020

Marekani yatoa tahadhari nyingine Tanzania kuhusu Covid-19

Mara ya mwisho kutolewa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya korona Tanzania ni Aprili 29


Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa ushauri mwengine wa tahadhari kwa raia wake wa Marekani kuhusu maambukizi ya virusi vya korona nchini humo.

Katika taarifa walioitia, ubalozi huo ulisema kuwa hatari ya kuweza kuambukizwa virusi hivyo jijini Dar es Salaam, bado ni kubwa, lakini haukutoa ushahidi wowote wa kuthibitisha madai hayo.

Taarifa hiyo imependekeza raia wake waepuke msongamano na wasitoke majumbani mwao.

Ushauri huo unatolewa siku chache baada ya wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kumwita kaimu balozi wa Marekani, Inmi Patterson, kupinga ushauri wa safari uliotolewa na ubalozi huo mwezi uliopita ambao unalingana na huu wa sasa.

Kwa taarifa zaidi, bonyeza link ifuatayo https://bbc.in/2U0Ey0L

No comments:

Post a Comment