Wednesday, 10 June 2020

Uganda yaandaa hospitali ya wazi yenye vitanda 40,000


Rais wa Uganda anataka wajiandae kwa ongezeko la maambukizi

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema nchi hiyo inaandaa hospitali ya sehemu ya wazi yenye vitanda 40,000 katika uwanja wa michezo wa Namboole uliopo mji mkuu, Kampala kwa ajili ya wagonjwa wenye virusi vya korona

Rais huyo amesema wizara ya Afya awali ilipanga kuweka vitanda 9,000 lakini aliagiza idadi hiyo iongezwe.

Uganda mpaka sasa ina idadi ya watu 657 wenye Covid-19, ugonjwa unaoathiri pumzi unaosababishwa na virusi vya korona.

Bw Museveni alisema nchi hiyo imefanikiwa kuzuia vifo vinavyohusiana na virusi vya korona lakini akaonya kwamba idadi inavyoongezeka na vifo vinaweza kutokea.

Alisema ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo miongoni mwa jamii, watu wanatakiwa kuwa makini zaidi na kukaa nyumbani kama hawana jambo la muhimu la kufanya.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment