Friday 5 June 2020

Waziri afukuzwa kwa kutaka kununua pipi za dola mil 2.2

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina

Waziri wa elimu wa Madagascar kafukuzwa kazi kutokana na mpango wake wa kuagiza pipi zenye thamani.

Rijasoa Andriamanana alisema wiki iliyopita alikuwa akiagiza pipi hizo kwa ajili ya watoto ili kutuliza ladha “chungu” ya dawa asili ya Covid, kulingana na shirika la habari la AFP.

Covid-Organics ni kitulizo kinachotumia mmea kinachopigwa chapuo na serikali ya nchi hiyo kama tiba ya Covid-19.

Kila mwanafunzi nchini humo alitarajiwa kupewa pipi tatu, kulingana na AFP.

Vyombo vya habari vya ndani vimesema waziri huyo alisimamisha mpango huo baada ya Rais Andry Rajoelina kukataa.

Kufukuzwa kwa waziri huyo kulitangazwa siku ya Alhamisi katika taarifa iliyosema mwenzake kwenye wizara ya elimu, Elia BĂ©atrice Assoumacou, atakaimu nafasi yake.

No comments:

Post a Comment