Wednesday, 14 January 2015

WAPEWA CHAKULA BURE KWA KUWA NA 'SURA NZURI'



The judging panel
Majaji wakiamua nani ana sura nzuri zaidi wa kupewa chakula cha bure


Wateja katika mkahawa mmoja unaofanya mapishi ya Korea, Zhengzhou, katika jimbo la Henan, wanapewa chakula cha bure iwapo atapigiwa kura kuwa miongoni mwa wenye sura nzuri.

Gazeti la mtandaoni la China Daily lilisema kundi la watu likifika kula hupigwa picha wanapowasili.

Hata hivyo, si wafanyakazi wa mkahawa huo uliopo China wanaoamua nani ana sura au mtindo mzuri wa nywele.

Kazi hiyo hufanywa na wafanyakazi kutoka kliniki moja ya upasuaji ya kubadilisha maumbile, ambao hutazama picha hizo na kuchagua tano bora.

Baadhi ya watu nchini humo wamefurahishwa na kupewa chakula bure lakini wengine walisema ni kuwavunjia watu heshima.

No comments:

Post a Comment