Saturday, 3 January 2015

LIBERIA YAACHA KUKATA MITI IPATE MISAADA



Man stands by deforested area

Liberia  inatarajiwa kuwa taifa la kwanza barani Afrika kuacha kukata miti yake kabisa na kwa kufanya hivyo wapate misaada ya kuendeleza nchi yao.

Norway itailipa nchi hiyo dola milioni 150 kufikia mwaka 2020 ili kuizuia isikate miti yake.

Kumekuwa na wasiwasi kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola utashawshi ongezeko la kukata miti katika nchi iliyo na shida sana ya fedha.

Maafisa wa Norway wamethibitisha kuwepo makubaliano hayo walipozungumza na BBC katika mkutano wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa mjini New York.

Misitu ya Liberia si mikubwa kama ilivyo kwenye nchi nyingine lakini ni sehemu muhimu iliyobaki ya msitu unaoleta mvua Afrika magharibi, huku takriban 43% ukiwa sehemu ya juu ya msitu wa Guinea.

Ni eneo lililo na aina mbalimbali ya wanyama dunaini, wakiwemo wanyama wa kipekee kama masokwe, tembo wa msituni na chui.

Lakini tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipomalizika mwaka 2003, ukataji miti kinyume cha sheria umevuka mipaka.


No comments:

Post a Comment