Saturday, 3 January 2015

WASANII WA HIP-HOP WANAOLIPWA ZAIDI 'CASH KINGS'

Dr. Dre
Dr Dre

Msemo "count up the cash" mwanzo wa wimbo wa Dr Dre wa Get Your Money Right bila shaka yana ukweli mtupu. 

Hatua yake ya kuiuzia kampuni ya Apple viskilizio vya masikioni (headphones) Beats, mapato yake ya dola milioni 620 katika kipindi cha miaka 12 iliyopita ni makubwa kuwahi kutokea kwa msanii yoyote aliyewahi kufanyiwa tathmini na Forbes.

Jumla ya kipato chake ni zaidi ya pesa kiduchu cha $60 milioni anachopata Jay Z, ambaye aliimba pamoja naye kwenye wimbo wa Get Your Money Right, na Diddy aliyeshika nafasi ya pili.

Kanye West
Kanye West hakufanikiwa kuwa tano bora


Taarifa zilizojiri, kipato cha Dr Dre ni zaidi ya kipato cha wote 24 walioorodheshwa.

Drake amechukua nafasi ya nne akiwa na dola milioni 33 jambo litakalomfurahisha sana, aliwahi kuiambia Forbes "Kama sipo kwenye orodha yenu, ntasikitika sana" mwaka 2013.

Macklemore & Ryan Lewis wa Seattle wenye kuwa na kipato cha dola milioni 32 wamechukua nafasi ya tano, akifuatiwa na Kanye West aliyezalisha dola milioni 30.

Pharrell Williams'
Pharell Williams, aliyetamba sana na kibao cha Happy ameshika nafasi ya tisa


Utajiri wa Birdman $24m, Lil Wayne $23m na $22m za Pharrell Williams unawaweka nafasi ya juu zaidi ya Eminem anaokadiriwa kuwa na utajiri wa takriban $18m na kukamilisha orodha ya 10 bora kwenye miondoko hiyo ya Hip-Hop.

Nicki Minaj ni mwanamke pekee kwenye orodha hiyo akiwa na kipato cha takriban dola milioni 14 licha ya kuondoka American Idol na kutofanya ziara za muziki. 

Ili kuwepo kwenye orodha hiyo, Forbes huangalia kipato kinachotokana kwenye ziara/shoo, mauzo ya rekodi zao, uchapishaji, mauzo ya vifaa mbalimbali nakadhalika.


No comments:

Post a Comment