Wednesday, 14 January 2015

ZAIDI YA MIILI 100 KUPATIKANA MTO GANGES, INDIA


 

Serikali nchini India inachunguza kupatikana kwa zaidi ya miili mia moja, iliyokutwa katika mto Ganges kaskazini mwa nchi hiyo.

Hakuna tuhuma za uhalifu zinazofikiriwa, lakini badala yake inaonekana miili hiyo, ambayo sasa imeharibika sana, iliachwa ielee katika mto huo, baada ya familia zao kushindwa kuwachoma moto kama taratibu za Wahindu zinavyotaka.

Waandishi wa eneo hilo walisema licha ya maiti kuonekana kwenye mto huo mara kwa marasi kawaida kuona miili ya watu wengi sehemu moja.

Kuna wasiwasi kuwa inasababisha matatizo makubwa kiafya na kuna taarifa kuwa hata wafanyakazi wa kufanya usafi waliokuwa wakitoa miili sasa wamekataa kuendelea.

Inasemwa kuwa idadi kubwa ya maiti zilizokuwa zikielea ni za watoto.

Chanzo: cbsnews.com

No comments:

Post a Comment