Thursday, 15 January 2015
HUDUMA YA AFYA ANGANI YAZINDULIWA KENYA
Kenya imezindua huduma yao ya kwanza ya gari la wagonjwa la angani itakayosaidia kuwahamisha majeshi ya usalama waliojeruhiwa kwenye mapambano.
Rais Uhuru Kenyatta alisema huduma hiyo ni muhimu kuhakikisha wanapata tiba haraka.
Huduma hiyo inatarajiwa kuwapa matumaini zaidi wafanyakazi wa masuala ya usalama wanaokabiliwa na vitisho vya mara kwa mara, mwandishi wa BBC alisema.
Baadhi ya wanajeshi na polisi wametoka damu mpaka kufa au kufa kutokana na ukosefu wa maji maeneo ya vijijini nchini Kenya kwasababu ya muda mrefu unaotumika kuwafikisha hospitalini.
Serikali ya nchi hiyo sasa imefanya makubaliano na Shirika la Msalaba Mwekundu, Red Cross na kampuni binafsi ya madaktari wasio na mipaka ya AMREF kutoa huduma za helikopta na magari wanapopata tu simu za kuhitaji huduma hiyo haraka.
Huduma hiyo pia itatolewa kwa wafanyakazi wa serikali, hasa wale wanaofanya kazi kwenye nyanja ya usalama vijijini na walio na vifaa vichache vya kutolea matibabu.
Kundi la Kisomali la al-Shabab limeongeza mashambulio nchini Kenya katika miaka ya hivi karibuni.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment