Sunday, 4 January 2015

KIFUNGO KWA KUMDHALILISHA RAIS KENYATTA


 A file photo taken on May 7, 2013 shows Kenyan President Uhuru Kenyatta (L) leaving a hotel in central London,
Okengo alikubali kosa la kumdhalilisha Rais Kenyatta

Mwanafunzi wa mwaka wa nne Chuo Kikuu Kenya amehukumiwa mwaka mmoja jela kwa kumdhalilisha Rais Uhuru Kenyatta kwenye mtandao wa kijamii.

Alan Wadi Okengo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye anajulikana pia kwa jina la lieutenant Wadi, lazima alipe faini ya  $2,200, au atumikie kifungo cha mwaka mwengine wa pili.

Ametiwa hatiani pia kwa kauli za chuki, baada ya kusema watu kutoka kabila la Kikuyu ambalo ndilo alilotoka rais huyo watengwe katika baadhi ya sehemu nchini humo.

Blogger maarufu alifunguliwa mashtaka hivi karibuni baada ya kumwita Bw Kenyatta "adolescent president".

Kenya ina wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii na mwandishi wa BBC nchini humo alisema kesi hiyo imezua mjadala mzito wa kipi kinaruhusiwa kwenye mitandao hiyo.

Mwandishi huyo alisema watu wengi wanahisi Okenga alivuka mipaka, kwa kuwa kauli zake zilikuwa na chuki binafsi na hazikutakiwa kuchapishwa.

Okenga alikiri makosa yote mawili, kauli za chuki na kumdhalilisha mkuu wa nchi.

Gazeti la Daily Nation kupitia mtandao wao limeripoti kuwa alikamatwa akiwa anajaribu kukimbia nchini humo.

No comments:

Post a Comment